Skip to main content

COVID-19 kuathiri elimu ya mamilioni ya watoto duniani kote

COVID-19 kuathiri elimu ya mamilioni ya watoto duniani kote

Pakua

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO limesema nchi 100 duniani zimefunga kabisa au kwa kiasi fulani shule na vituo vya elimu na kuwakoseha mamilioni ya watoto masomo, kwa sababu ya mlipuko wa COVID-19 unaoendelea. Grace Kaneiya na taarifa zaidi
(TAARIFA YA GRACE)
Shirika hilo sasa linasema hivi sasa linazisaidia nchi kusala suluhu ya jinsi ya Watoto kuweza kusoma wakiwa nje ya mazingira ya shule ikiwemo kupitia mtandaoni na nyenzo zingine za kidijitali
Kwa mujibu wa UNESCO nchi 85 zimefunga shule katika nchi nzima ili kujaribu kudhibiti maambukizi ya virusi hivyo vipya vya Corona. Hatua hizo zimewaathiri Watoto na vijana zaidi ya milioni 776.7.
Akizungumza na UN News kwa njia ya simu kutoka mjini Brussels nchini Ubelgiji mwakilishi wa UNESCO nchini humo Vincent Defourny amesema UNESCO inashirikiana kwa karibu na serikali ili kutekeleza mapendezo ya matumizi ya teknolojia.
“UNESCO inashauri kupunguza athari kwa mitaala ya shule kwa njia mbalimbali. Kitu cha kwanza ni kutumia rasilimali zote zilizopo za kuwezesha kusoma wakiwa mbali ambazo zinaweza kuwa ni kupitia mtandao wa intaneti, radio, televisheni na njia zingine zote zinazoruhusu kusoma ukiwa mbali”
Ameongeza kuwa nchi zipatazo 15 zimefunga shule kwa sehemu fulani . endapo hatua hizo zitatekelezwa katika ngazi ya kitaifa basi itawaacha wanafunzi wengine mamilioni bila kuhudhuria madarasa mesema Defourny na kuongeza kuwa “ni  muhimu na lazima kuchukulia maamuzi haya kwa kila hali ili yatekelezeke.”
Kama sehemu ya hatua za kupunguza kusambaa kwa virusi vya Corona UNUESCO inasaidia hatua zinazochukuliwa na nchi kupunguza athari katika mifumo ya elimu na kuwezesha masomo kuendelea hususani kwa wale wasiojiweza.
UNESCO inasema kufunga shule hata kama ni kwa muda mfupi kunakuja na gharama kubwa za kijamii na kiuchumi. Na kubwa zaidi ni fursa ndogo sana za kuku ana kujiendeleza.
Na katika upande wa lishe shirika hilo linasema kufunga shule kunasababisha Watoto wengi kukosa mlo ambao mara nyingi huupata shuleni. Lakini pia inasema wazazi walio na uwezo mdogo wa kuhakikisha Watoto wao wanaweza kusoma wakiwa mbali wanaweza kukabiliwa na athari za kutokuwa na nyezo za kidijitali kuwezesha hilo.
Na mbali ya hayo UNESCO imeonya kwamba Watoto wengi wanaweza kuwa katika hatari ya kupata tabia mbaya kwa kuachwa nyumbani pekee yao.

 

Audio Credit
Assumpta Massoi/ Grace Kaneiya
Audio Duration
2'37"
Photo Credit
World Bank/Arne Hoel