Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO imetuepusha na kilimo cha mazoea- Wanawake Kakonko

FAO imetuepusha na kilimo cha mazoea- Wanawake Kakonko

Pakua

Mkoani Kigoma nchini Tanzania hususan katika kata ya Katanga wilayani Kakonko, ushirikiano kati ya serikali na Umoja wa Mataifa kwenye kuhakikisha wakulima wanahimili mabadiliko ya tabianchi umeanza kuzaa matunda. Ushirikiano huo unaosongeshwa na wananchi wenyewe kwa ubia na shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO ni katika kuwapatia wakulima mbinu bora za kilimo ili kuwepo na uhakika wa chakula. Assumpta Massoi wa UNNews Kiswahili alitembelea kata hiyo na kukutana na wanawake waliounda kikundi ili kupokea mafunzo hayo kwa pamoja na kutekeleza kwa vitendo kupitia shamba darasa. Je ni nini wanafanya? Fuatana naye basi kwenye makala hii ambapo kiongozi wa kikundi hicho cha Umoja anaanza kwa kujitambulisha.

 

Audio Credit
Grace Kaneiya/ Assumpta Massoi
Audio Duration
4'17"
Photo Credit
UN News/Assumpta Massoi