Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Stadi kutoka UNHCR zaleta nuru kwa wakimbizi

Stadi kutoka UNHCR zaleta nuru kwa wakimbizi

Pakua

Kutafuta suluhu ya kudumu kwa ajili ya mahitaji ya wakimbizi na wasaka hifadhi kunahitaji ushiriki wa sekta zote katika jamii. Vipaji bila mipaka ni mfano mzuri wa mfumo jumuishi ambapo serikali, sekta binafsi na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR wanafanya kazi kwa pamoja kujumuisha wakimbizi katika ajira.  Grace Kaneiya na ripoti kamili.

Kutana na mkimbizi Delsy kutoka Colombia, Delsy alikimbilia Panama miaka 18 iliyopita, ambapo ndoto yake ya kufanya kazi katika mitindo ilididimia lakini kufuatia programu ya kuwaweka wakimbizi wenye stadi kwenye ajira, sasa anamatumaini.

Mkimbizi Delsy anaelezea kilichosababisha wao kukimbia,“Maisha yetu yalikuwa hatarini kwa sababu ya makundi yaliyojihami, mume wangu alilazimika kuondoka kwanza kwa ajili ya kuokoa maisha yake.”

Programu ya vipaji bila mipaka ilianzishwa na UNHCR na wadau wake kwa lengo la kuimsrisha fursa za wakimbizi na vijana mashinani katika kupata nafasi za ajira.

Programu hiyo sio tu inawasaidia wakimbizi kuimarisha stadi zao na kuelezewa kuhusu fursa zilizopo lakini pia wanaelimishwa kuhusu haki zao na majukumu yao chini ya sheria za kazi za nchi husika. Baada ya kumaliza program hiyo wakimbizi wanasaidiwa mpaka pale watakapopata ajira. Dagmar Garcia, ni mmiliki wa duka la nguo za kushonwa, “Wakimbizi wanachangia kwa kiasi kikubwa katika soko la ajira na biashara, kufanya kazi na Delsy imekuwa ni jambo jema.”

Tangu kuanza kwa programu hiyo mwaka 2018, wakimbizi 214 na waomba hifadhi na Wapanama wamepokea vyeti baada ya kukamilisha mafunzo ambapo asilimia 50 ya wakimbizi waliopokea mafunzo wana kazi nzuri na wameimarisha kipato cha familia kwa asilimia 65.

Kufikia mwaka 2018 Panama ilikuw ainahifadhi wakimbizi 1,691 na waomba hifadhi 1,791 kutoka Colombia.

 

Audio Credit
Anold Kayanda/Grace Kaneiya
Audio Duration
2'6"
Photo Credit
Picha/UN-Habitat/Julius Mwelu