Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ufadhili kwa ajili ya SDGs unakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo za kisiasa-UNCTAD

Ufadhili kwa ajili ya SDGs unakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo za kisiasa-UNCTAD

Pakua

Ripoti ya mwaka 2019 kuhusu kuwekeza kwa ajili ya maendeleo endelevu ya kikosi kazi cha mashirika mbali mbali kuhusu uwekezaji kwa ajili ya maendeleo inaonya kwamba kuchangisha fedha zinazohitajika kwa ajili ya kutekeleza ajenda ya mwaka 2030 ya maendeleo endelevu inasalia kuwa changamoto.

Licha ya kwamba kuna ishara za mafanikio, lakini uwekezaji ambao ni muhimu katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu, SDGs bado hayajafadhiliwa ipasavyo na mifumo ya kimataifa inakabiliwa na wakati mgumu.

Kauli hiyo inaendana na mtazamo wa kamati ya biashara na maendeleo  ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD ambako Katibu Mkuu wake katika mahojiano ya awali na Assumpta Massoi ameangazia mazingira ya sasa ya kisiasa na changamoto zingine zinazokwamisha ufadhili wa SDGs

Audio Credit
Assumpta Massoi/ Mukhisa Kituyi
Audio Duration
3'48"
Photo Credit
UN News/Grece Kaneiya