Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkimbizi Ould asema siku zote baada ya dhiki ni faraja:

Mkimbizi Ould asema siku zote baada ya dhiki ni faraja:

Pakua

Kutana na Sidi Ould Amin, raia wa Mali aliyekimbia nchi yake hiyo hadi Burkina Faso, lakini sasa amerejea nyumbani na kuanzisha biashara ya ufundi cherahani, kwa kutumia ujuzi alioupata kupitia mafunzo ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR akiwa kwenye kambi ya wakimbizi nchini Mali. Jason Nyakundi na taarifa zaidi.

Mjini Mpoti Mali Sid Ould Amin mwenye umri wa miaka 37 akiwa nyumbani kwake na familia yake baada ya kurejea kutoka ukimbizi nchini Burkina Faso alikokimbilia mwaka 2012 baada ya vita kuzuka nchini Mali na kupoteza kila kitu akisema, "tumekuwa masikini wa kutupa, kabla ya vita tulikuwa vizuri, lakini baada ya zahma hii, uharibifu, wizi, na mashambulizi hatua chochote kilichosalia. »

Tangu mwaka 2012 zaidi ya watu 130,000 wamefungasha virago Mali na kukimbia vita akisema kuwa,  "sikutaka kuondoka lakini unapolazimika inabidi uondoke.Ukiona kinachoendelea basi huna budi kuondoka "

Kwenye kambi ya wakimbizi alikokimbilia Burkina Faso Ould alipatiwa msaada, ulinzi na hata mafunzo yanayotolewa na UNHCR ikiwemo utengenezaji wa sabuni, ufundi makenika na ufundi cherahani akieleza kuwa, 

 "nilipoambiwa kwamba mafunzo ya ufundi cherahani yapo, nikasema hayo ndio ninayoyapendelea kufanya kwa sababu nguo za watoto wangu nyumbani zimechanika."

Mwaka 2017 Ould aliamua kurejea nyumbani Mali na kufungua biashara ya ufundi cherahani, kwake ametimiza ndoto kwani baada ya dhiki ni faraja na sasa anatoa shukran kwa jamii yake kwa kuwafundisha vijana wasichana kwa wavulana ambao ni watoto wa mitaani mafunzo ya ushonaji ili waachane ta hulka ya kuombaomba mitaani

Audio Duration
1'46"
Photo Credit
UNICEF/Keïta