Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mama bodaboda: Usiache mila na desturi zikazima ndoto zako.

Mama bodaboda: Usiache mila na desturi zikazima ndoto zako.

Pakua

Kutana na mwanamke wa shoka Palagie Gerald ali maarufu kama mama bodaboda kutoka nchini Kenya anayesema hakuna kazi ya mwanaume wala mwanamke ukidhamiria, kulikoni?.

Pelagie ni mke, mama na sasa ni mwendesha pikipiki mashuhuri kama bodaboda kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya, ambaye hakuacha mila na desturi za mfumo dume kumzuia kufanya atakalo, "Watu mitaani wananiita mama boda boda, sasa hiyo ni kama nimezoea na naona ni kawaida."

Usafiri wa bodaboda ni maarufu sana hasa kwa kuwa ni rahisi na wengi wanaumudu na katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma umekuwa chanzo kikubwa cha kipato ikiwepo kwa Palagie ambaye anajiamini licha cha changamoto za kazi hiyo, "Nimejiamini na kujiskia kwamba nitatembeza vizuri na niko na nguvu. Mwanaume anaweza penda nimbebe kwa sababu anajua najali maisha ya abiria ambaye nimembeba, niendeshe polepole na nihakikishe amefika salama aendapo."

Lakini kila uchao anakabiliwa na vikwazo katika jamii, "kuna wale wananivunja moyo eti  mama kwanini unafanya kazi ya wanaume lakini najipa moyo nikiendelea. Akina mama kujeni tuwe pamoja kwa sababu kwa dunia ya sasa hamna kazi ya mwanamke au mwanamume, tunafaa kushirikiana kwa pamoja na kufanya kazi kwa pamoja bila kujali hii ni kazi ya mwanaume au hii ni kazi ya mwanamke." 

Kwa Palagie ni aluta kontinua mapambano ya usawa wa kijinsia yanaendelea na kwake kazi ni kazi bora mkono wende kinywani.

Audio Credit
Jason Nyakundi
Audio Duration
1'31"
Photo Credit
Benki ya Dunia/Stephan Gladieu