Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Linalowezekana kufanyika kujipatia kipato fanya usibweteke:Wanawake Dodoma

Linalowezekana kufanyika kujipatia kipato fanya usibweteke:Wanawake Dodoma

Pakua

Kazi za kuajiriwa ofisini imekuwa mtihani mkubwa kwa wanawake wengi hususan barani Afrika, na ujasiriamali umekuwa ndio kimbilio na mkombozi kwa waliosoma na hata wasio na elimu kwani kinachohitajika ni juhudi na maafifa. Hii ni moja ya kauli zilizotolewa na wanawake wajasiriamali kutoka mkoani Dodoma nchini Tanzania wanaojiuhusisha na kazi mbalimbali ikiwemo za udereva wa pikipiki ya magudurudumu matatu ali maarufu kama Bajaji. Wanawake hawa wanasema mwanamke ili kujikwamua kiuchumi pamoja na kuwezeshwa iwe na mikopo au fedha katika kikundi, mchango wako binafsi wa nguvukazi na juhudi unahitajika . Kuwasikia kwa udani wanawake hao tuungane na Devotha Songorwa kutoka Radio washirika Tanzania Kidstime FM. Mkoani Dodoma.

Audio Credit
Devotha Songorwa
Audio Duration
3'24"
Photo Credit
UN News/Assumpta Massoi