Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake kupata mafunzo kutoka chama cha wanahabari wanawake Tanzania,

Wanawake kupata mafunzo kutoka chama cha wanahabari wanawake Tanzania,

Pakua

Mafunzo kutoka TAMWA-Zanzibar yawezesha wanawake wa Kidoti, Kaskazini A

Huko Zanzibar, Tanzania mafunzo yaliyotolewa na chama cha wanahabari wanawake Tanzania, TAMWA kuhusu kuweka na kukopa yamewezesha wanachama wake ambao ni wanawake wakazi wa eneo la Kidoti, wilaya ya kaskazini A, kuweza kujiinua kiuchumi. Assumpta Massoi na ripoti kamili.

(Taarifa ya Assumpta Massoi)

Eneo la Kidoti, Wilaya ya Kaskazini A, kisiwani Unguja,  Zanzibar nchini Tanzania nakutana na wanakikundi cha Mwanzo Mgumu chenye wanachama 20.

Mafunzo kutoka chama cha wanahabari wanawake, Tanzania, TAMWA tawi la Zanzibar, kuhusu kuweka na kukopa yamewajengea uwezo wa kuweza hata kukopeshana na kufanya biashara.

Mchana huu nimekuta wanakikundi wakiwa katika siku ya kuweka hisa zao.

Kuna kikoba cha fedha za kukopeshana na pia mfuko wa Jamii kwa ajili ya shughuli za kifamilia kama vile harusi au msiba.

Mwenyekiti wa kikundi hiki Fatuma Ally Heri akafunguka.

Fedha wanazokopeshana kutoka kwenye hisa huzitumia kuanzisha mradi kama anavyoelezea mwanachama huyu.

Hadi sasa mfuko wao walioanzisha miezi takribani 9 iliyopita sasa una zaidi ya shilingi Laki Nane.

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
2'52"
Photo Credit
UN News/Assumpta Massoi