Mwanamke Mjasiriamali Ester Damiani anayeponda mawe kuwa kokoto,Tanzania
Pakua
Wakati tukielekea kuadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake tarehe 8 ya mwezi huu ambapo kaulimbiu yaa mwaka huu inaangazia kizazi cha usawa, yaani kizazi ambacho mwanamke habaki nyuma.
Licha ya wanawake wengi kuathiriwa na imani ya kuwa kuna kazi za kiume na za kike wapo baadhi ambao wameamua kuithibitishia jamii kuwa dhana hiyo ni potofu. Mathalani Ester Damiani mwenyeji wa Kakonko mkoani Kigoma ambaye kwa sasa yuko wilayani kahama mkoani shinyanga akitafuta riziki, kwa miaka 10 anajishughulisha na ujasiliamali wa kuponda mawe kuwa kokoto na kazi hii anasema anaipenda sana kama alivyozungumza na PAULINA MPIWA wa radio washirika Huheso Fm ya wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Audio Credit
GRACE KANEYA
Audio Duration
6'17"