Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Karanga tu ndio mlo wetu wa sasa- Wakazi Nzara

Karanga tu ndio mlo wetu wa sasa- Wakazi Nzara

Pakua

Wakati Sudan kusini ikiendelea kupambana kuimarisha amani, wakazi wa eneo la Nzara wamekumbwa na janga la moto wa nyika ambao umeteketeza takribani ardhi yenye ukubwa wa maili tano za mraba katika jimbo la Equatoria Magharibi na kuwaacha mamia ya watu bila makazi, umesema  mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS. Brenda Mbaitsa na taarifa zaidi

(TAARIFA YA BRENDA MBAITSA)

UNMISS imesema moto huo umeteketeza nyumba za Tukul ambazo ni nyumba za asili za eneo hilo, mifugo na kupoteza maisha ya mtu mmoja. 

Fatina Thomas mkazi wa Nzara na ni mmoja wa manusura wa moto huo

(Sauti ya Fatina Thomas-)

“Tunaishi nje tu. Tuna karanga tu kwa ajili ya chakula. Kila kitu kimeungua, tuko tu nje ya nyumba zetu zilizoteketea.”

Afisa wa UNMISS Stella Folasade Abayomi, ambaye anahusika na  masuala ya jamii mjini Yambio anasema madhara ya moto huo yanatisha.

(Sauti ya Stella Folasade Abayomi-)

 “Wanajamii wengi wametawanywa. Watu wengi hawana makazi, wamehama. Wengi wameripoti kupoteza mali zao na kimsingi vyanzo vyao vya mapato maana hapa wengi ni wakulima. Mashamba yameungua na wamepoteza vyakula vyao vyote katika maghala. Kwa hivyo kutokana na kile tunachokiona, nafikiri kuna umuhimu wa haraka wa msaada wa kibinadamu kuwasaidia watu kwa kuwapatia makazi ya muda, mahema, chakula na bila shaka vitu vingine ambavyo si chakula.”

Audio Credit
Flora Nducha/Brenda Mbaitsa
Audio Duration
1'33"
Photo Credit
UNMISS