Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO ikitaka nchi zifunguke kuhusu Corona, huko Afrika Mashariki mataifa ikiwemo Kenya, yamejiandaa

WHO ikitaka nchi zifunguke kuhusu Corona, huko Afrika Mashariki mataifa ikiwemo Kenya, yamejiandaa

Pakua

Shirika la afya  ulimwenguni, WHO limesema kuwa changamoto kubwa hivi sasa katika kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona au COVID19, ni nchi nyingine zenye wagonjwa hao kutokuwa tayari kuwasilisha taarifa zao kwa shirika hilo.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Gebreyesus amesema hayo leo wakati wa mkutano wake wa kila siku na waandishi wa habari huko Geneva, Uswisi wenye lengo la kutoa muhtasari wa hali ilivyo kuhusu ugonjwa huo. Huku wito ukisistizwa kwa nchi kuendelea na maandalizi ya kukabiliana na mlipuko huo endapo utazuka. Ili kufahamu kwa nchi za Afrika ya Mashariki maandalizi yakoje nimezungumza na Dkt. Peter Borus afisa ya kisayansi wa WHO akiwa mjini Nairobi Kenya

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
2'30"
Photo Credit
UNICEF/Hendrik Hildelbrandt