Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COVID-19 yaweza kuwa na madhara ya kiuchumi hata nje ya China- IMF

COVID-19 yaweza kuwa na madhara ya kiuchumi hata nje ya China- IMF

Pakua

Wakati idadi ya maambukizi ya virusi vya corona COVID-19 ikiendelea kuongezeka kila uchao, Shirika la afya ulimwenguni, WHO limehimiza jamii ya kimataifa kuwekeza katika suluhu za afya ambazo zinaweza kusaidia katika kudhibiti mlipuko wa ugonjwa huo sasa na wakati huo huo kusaidia katika kujiandaa kwa ajili ya kuwekeza katika jamii kwa siku za usoni. Grace Kaneiya na ripoti kamili.

Wito huo umetolewa siku chache baada ya taarifa za shirika la fedha duniani, IMF ya makadirio yake kuhusu athari za mlipuko wa virusi vya corona kiuchumi. 

Mkurugenzi Mkuu wa IMF, Kristalina Georgieva amesema ni muhimu kukumbuka kwamba..

(Sauti ya Kristalina)

“Kuhusu hali ilivyo sasa, huenda hali tuli nayo sasa ni athari za muundo wa herufi V, kwa maana kuwa kutakuwa na kushuka kwa shughuli za kiuchumi nchini China ikifuatiwa na kuibuka kwa haraka na athari kwa China zikadhibitiwa. Kwa mantiki hiyo athari kwa uchumi wa dunia pia zitadhibitiwa.”

Hata hivyo Mkurugenzi Mkuu huyo amesema hali ya China na uchumi wa dunia kwa sasa ni tofauti kuliko ilivyokuwa wakati wa mlipuko wa homa ya mafua, SARS.

(Sauti ya Kristalina)

“Uchumi wa China ni muhimu kwa dunia. Wakati huo ilikuwa asilimia 8 ya uchumi wa dunia. Sasa ni asilimia 19 na sasa ina uhusiano zaidi kwa Asia na dunia  nzima. Kwa hiyo, tafrani huenda zikashuka chini na kufika hadi nchi zingine. Na tatu uchumi wa dunia katika miaka ya mwanzo wa 2,000 ilikuwa katika nafasi nzuri lakini leo tunakadiria ukuaji mdogo zaidi wa asilimia 3.3 kimataifa. NI ukuaji mdogo baada ya kushuka katika kipindi cha mwaka mmoja. Kufuatia sababu hizo, ni lazima tufuatilie ni nini athari na kugeuza hali ya sasa kuwa makadirio.”

Kwa mujibu wa WHO idadi ya vifo kutokana na vifo nchini China ni 2,118 na visa 74,576 kote nchini.

Audio Credit
Assumpta Massoi/Grace Kaneiya
Audio Duration
2'30"
Photo Credit
UN News/Jing Zhang