14 FEBRUARI 2020

14 Februari 2020

Leo siku ya wapendanao Duniani katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa Anold Kayanda anakuletea

-Wahamiaji 11,500 walikwenda Yemen kila mwezi kutoka Pembe ya afrika mwaka jana limesema shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM

-WFP inaendelea kutoa msaada wa chakula cha dharura kwa watu ambao wako katika uhitaji mkubwa kaskazini magharibi mwa Syria licha ya uhasama ulioongezeka ambao wiki hii ulisababisha kusimamisha usambazaji wa misaada kwa saa 24. 

-Na Mtaalamu  huru aliyeteuliwa na Baraza la haki za binadamu,  Michael Lynk, amepongeza hatua ya kuachiliwa kwa taarifa kuhusu makampuni ya biashara yanayohusikana na shughuli zinazohusiana na makazi ya  walowezi Jerusalem Mashariki na ukingo wa Magaharibi akisema kuwa hiyo ni hatua muhimu ya mwanzo ya uwajibikaji.

-Mada kwa kina leo inajikita na wauguzi na wakunga , tutakuwa nchini Tanzania

-Na katika kujifunza Kiswahili mtaalam wetu Onni Sigalla anafafanua maana ya neno "Halifu"

Audio Credit:
UN News/Anold Kayanda
Audio Duration:
10'43"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud