Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Huduma tunazozitoa sisi wauguzi zimepunguza sana magonjwa Pangani

Huduma tunazozitoa sisi wauguzi zimepunguza sana magonjwa Pangani

Pakua

Kazi ya uuguzi ina panda shuka zake kama zilivyo kazi nyingine lakini kinachotufanya tuendelee kusonga mbele ni pale tunapoona watu wamepona na wameelimika kuhusu afya zao. Ni kauli ya Vailet Prosper ambaye amefanya kazi kwa muda mrefu katika Hospitali ya Pangani mkoani Tanga Tanzania. Vailet anafanya kazi ya uuguzi na ukunga ambayo mwaka huu inaenziwa na shirika la afya duniani WHO kuwa ni miongoni mwa kazi muhimu katika ustawi wa afya ya binadamu ambayo ina uhusiano wa moja kwa moja na maendeleo endelevu. Basi tuungane na Saa Zumo wa redio washirika Pangani FM, katika mahojiano haya na muuguzi Vailet Prosper.  

Audio Credit
Grace Kaneiya/ Saa Zumo/ Vailet Prosper
Sauti
3'55"
Photo Credit
© UNICEF