12 FEBRUARI 2020

12 Februari 2020

Katika Jarida la Habari hii leo anold Kayanda kutoka Umoja wa Mataifa anakuletea

-Shirika la afya ulimwenguni WHO leo limetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kutousahau ugonjwa wa Ebola pamoja na kwamba inakabiliana na virusi vya Corona hivi sasa kwani kufanya hiyo itakuwa kosa la jinai lenye madhara makubwa ya kibinadamu

-Mradi wa UNICEF wa mafunzo kwa waendesha boda boda ni nuru kwa wanawake wajawazito na watoto wagonjwa nchini Uganda

-Ubora wa miji ni pamoja na urahisi wa usafiri limesema shirika la Umoja wa Mataifa la makazi UN-HABITAT katika uzinduzi wa sanam ya mradi wa kuchagiza matumizi ya baiskeli huko Abu Dhabi kwenye kongamano la kumi la kimataifa la miji WUF10

-Makala yetu leo inaendelea na mfululizo wa wauguzi na wakunga tuko Tanga Tanzania kwa muuguzi wa hospitali ya Pangani anasemaje sikiliza

-Na mashinani tunakutana na mkurugenzi mtendaji wa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP Inger Anderson akichagiza kuhusu utimizaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDGs

Audio Credit:
UN News/Anold Kayanda
Audio Duration:
11'36"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud