Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kumbukumbu na mikakati ya kupambana na nzige, Uganda

Kumbukumbu na mikakati ya kupambana na nzige, Uganda

Pakua

Wakati shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limeonya juu ya janga la njaa katika ukanda wa Africa Mashariki  na pembe ya Afrika kutokana na uvamizi wa nzige nchini Ethiopia, Somalia na Kenya. Nchini Uganda hofu inazidi kutanda wakati ambapo nzige hao waperipotiwa kuvamia maeneo ya mpaka wake na Kenya, na kuharibu mazao ya kilimo na mimea katika mamilioni ya ekari. FAO imeitahadharisha Uganda na Sudan Kusini kuwa makini na kuchukua hatua ili kukabiliana na wimbi hilo la nzige endapo litazuka. Kutokana na onyo hilo Uganda imeibua kumbukumbu za madhara ya nzige miaka takribani 70 iliopita katika maeneo ya mpaka wake na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,DRC. 

Audio Credit
UN News/John Kibego
Audio Duration
3'48"
Photo Credit
UNEP GRID Arendal/Peter Prokosch