Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lengo letu ni kuhakikisha kwamba wanawake na wasichana wanaonekana kidijitali-Sambuli

Lengo letu ni kuhakikisha kwamba wanawake na wasichana wanaonekana kidijitali-Sambuli

Pakua

Kwa miaka mingi, wanawake walikuwa wakiachwa nyuma katika maendeleo na hata maswala ya kijamii ikichochewa na utamaduni na mitazamo dume kwenye jamii. Kwa kutambua hilo Umoja wa Mataifa kupitia lengo namba tano la malengo ya maendeleo endelevu linalenga kuziba pengo hilo ambalo kwa miaka limebinya haki za wanawake na wasichana. Moja ya maeneo ambako mwanamke ameachwa nyuma ni ulimwengu wa dijitali na kwa kutambua hilo Katibu Mkuu aliunda jopo maalum kwa ajili ya kusongesha malengo hayo mbele. Mmoja wa wajumbe hao ni Nanjira Sambuli  ambaye pia ni meneja wa masuala ya será katika mfuko wa kimataifa,  world wide web Foundation ambapo katika mazungumzo ya awali alimwambia Flora Nducha kuhusu ujumuishaji wa wanawake katika zama za kidijitali.

Audio Credit
UN News/Flora Nducha
Audio Duration
3'39"
Photo Credit
UN News/Patrick Newman