13 JANUARI 2020
Katika Jarida la Habari hii leo Grace Kaneiya anakuletea
-Miaka 10 baada ya tetemeko baya la ardhi nchini Haiti athari zake zinaendelea kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM
-Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limeutenga mwaka 2020 kuwa ni wa afya ya mimea kwa kutambua mchango na thamani ya mimea hiyo kwa maisha ya watu na syari dunia
-Maelfu ya Wavenezuela wakiwemo watoto wanaendelea kufungasha virago na kukimbilia nchi jirani ikiwemo Brazil limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF
-Makala yetu leo inatupeleka Tanzania ambako mabadiliko ya tabianchi na shuhguli za kibinadamu vinasababisha kupungua kwa ukubwa wa ziwa Tanganyika
-Na mashinani leo tunapata ujumbe kutoka kwa Bw. Evans Siangicha Mratibu wa shughuli za Umoja wa Mataifa mkoani Kigoma nchini Tanzania.