Ikiwa imesalia takribani miaka kumi kufikia mwaka 2030 ambao umepangwa kuwa mwaka ambao malengo 17 ya maendeleo endelevu, SDGs yatakuwa yametimizwa. Juhudi kote duniani zinaendelea kuhakikisha lengo hilo linafikiwa. Nchini Tanzania, msichana mbunifu Jonatha Joram anayeishi katika jiji la Dar es Salaam ameamua kushiriki katika utunzaji wa mazingira kwa kurejeleza bidhaa ambazo tayari zimetumika ili ziweze kutumika tena badala ya kutupwa na kuchafua mazingira. Katika mahojiano haya na Anold Kayanda wa UN News, Jonatha anaanza kwa kueleza anavyozifanya shughuli zake