Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake wapigania nafasi katika sekta ya mafuta, Turkana Kenya

Wanawake wapigania nafasi katika sekta ya mafuta, Turkana Kenya

Pakua

Katika eno la Turkana nchini Kenya shughuli za uchimbaji wa mafuta zimeshika kasi, lakini kama ilivyo sehemu nyingi duniani kuna baadhi ya kazi ikiwemo ya uchimbaji mafuta zimekuwa zikichukuliwa kama ni kazi za wanaume. Lakini kwa wanawake wa Turkana wanasema hapana , kila kazi inaweza kufanywa na kila mtu endapo fursa inatolewa na jitihada zinafanyika. Na  matakwa ya wanawake hao ni kuweza kushiriki katika sekta hiyo yenye manufaa kwani uhusisha uwekezaji wa mabilioni ya dola za kimarekani. Umoja wa Mataifa umekuwa ukipiga debe la uwezeshaji wanawake kuanzia katika ngazi za kijamii hadi kwenye utawala kwani hilo litasaidia kuziba pengo la umasikini na kusongesha mbele ajenda ya maendeleo endelevu  ifikapo 2030. Sasa leo katika makala hii mwandishi wetu John Kibego amezungmuza na wanawake hao wa mashinani na kishsa Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Friends of Lake Turkana ambaye ni mzaliwa wa jamii hiyo kuhusu ushiriki wao katika sekta ya mafuta, ungana nao.

Audio Credit
Brenda Mbaitsa/ John Kibego
Sauti
4'7"
Photo Credit
UN-Habitat/Julius Mwelu