26 DESEMBA 2019

26 Disemba 2019

Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Grace Kaneiya anakuletea

-Daktari bingwa wa masuala ya wanawake nchini Congo DRC, Denis Mukwege amewataka watu walioathirika na kubakwa kutambua kuwa sio kosa lao bali wao ni waathirika na lazima wahakikishe wahusika wanafikishwa kwenye vyombo vya sheria

-Mkimbizi kutoka Syria aliyefungasha virago mara tano kuingia Iraq anasema sasa basi imetosha na amechoka kukimbia

-Nchini Tanzania kutana na Jonatha Joram binti mwanaharakati wa mazingira anayetumia nguo chakavu kutengeneza bidhaa mbadala kujipatia kipato na kulinda mazingira

-Makala yetu leo inatupeleka Tanzania kwa kijana Richard Katuma  ambaye kwa wakati mmoja alikuwa anachangia katika vipindi vyetu

-Na mashinani unapata ujumbe kutoka kwa Bi. Maria Jose Alcala Donegani, mshauri mwandamizi wa masuala ya jinsia kutoka shirika la Umoja wa Mataifa linalopambana na ukimwi UNAIDS.

 

 

Audio Credit:
UN News/Grace Kaneiya
Audio Duration:
11'30"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud