24 DESEMBA 2019

24 Disemba 2019

Katika Jarida la Habari hii leo Grace Kaneiya anakuletea

-Watoto waendelea kubeba gharama ya vita nchini Syria hususan katika jimbo la Idlib limeonya leo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF

-Baada ya madhila na shulba chungunzima kwenye mahabusu nchini Libya mkimbizi kutoka Darfur aliyehamishiwa Rwanda asilmulia kilichomsifu na furaha yake sasa

-Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR ujulikanao kama MINUSCA kwa kushirikiana na serikali waanzisha mafunzo ya ufundi kwa raia ili wajipatie kipato na kuleta utangamano katika jamii

- Makala yetu leo inatupeleka Kajiado Kenya kwenye kituo cha Beyond Hope ambacho ni kimbilio la wasichana wanaokimbia ndoa za utotoni

-Na mashinani tunaangazia kazi ya shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wahamiaji IOM kwenye eneo la Darfur nchini Sudan

Audio Credit:
UN News/Grace Kaneiya
Audio Duration:
11'26"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud