23 DESEMBA 2019

23 Disemba 2019

Katika Jarida la Habari hii leo Grace Kaneiya anakuletea 

-Nchi tatu za Afrika ambazo ni Kenya, Msumbiji na Niger leo zimetangazwa na shirika la afya ulimwenguni kufanikiwa kudhibiti milipuko ya polio

-Ecuador imetakiwa na wataalam wa haki za binadamu kuhakikisha inakomesha ubaguzi wa rangi na madhila yanayowakabili raia wake wenye asili ya Afrika

-Nchini Uganda mafunzo ya kutumia roboti yanayofadhiliwa na Benki ya Dunia yaleta mwamko wa teknolojia mashuleni

-Makala yetu leo inatupeleka Kenya kwa mkurugenzi wa NEMA kumulika uchafuzi wa hewa unaosababishwa na usafiri wa Umma jijini Nairobi.

-Na mashinani leo inatupeleka kwenye kambi ya wakimbizi Mali kwa binti aliyenufaika na mafunzo ya topografia yanayotolewa na Umoja wa Mataifa

Audio Credit:
UN News/Grace Kaneiya
Audio Duration:
10'42"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud