20 DESEMBA 2019

20 Disemba 2019

Katika Jarida la mada kwa kina hii leo Anold Kayanda anakuletea

-Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amekutana na Papa Mtakatifu Francis na kujadili mengi ikiwemo kauli za chuki, haki za binadamu na maadhimisho ya amani ya sikukuu za Chrismas na mwaka mpya

-Hali imeelezwa kuendelea kuzorota katika vituo wanavyoshikiliwa wakimbizi na wahamiaji nchini Libya,

-Dola milioni 34 zinahitajika kunusuru maisha ya watu zaidi ya 260,000 wanaokabiliwa na hali mbaya ya kutokuwa na uhakika wa chakula nchini Lesotho limesema shirika la OCHA

-Mada kwa kina leo inajikita na mchango wa wanawake katika operesheni za amani za Umoja wa Mataifa utamsikia Meja Veronica Owuor kutoka Kenya  akizungumza na Flora Nducha 

-Na katika kujifunza Kiswahili leo mchambuzi wetu Onni Sigalla kutoka BAKITA nchini Tanzania anafafanua maana ya neno "DEDE"

Audio Credit:
UN News/ Arnold Kayanda
Audio Duration:
9'58"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud