Je wafahamu kuwa usajili wa vizazi bado ni tatizo kubwa hasa kwa nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara? Kama sivyo basi fuatana nasi katika ripoti ya leo ya UNICEF kuwa watoto wakizaliwa hawasajili na hili ni tatizo. Kisha ni Tanzania kwake Balozi Augustine Mahiga, Waziri wa Katiba na Mambo ya Sheria akizungumzia Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini humo na umuhimu wa kuhakikisha utamaduni na maadili ya nchi yanazingatiwa. Tunabisha hodi pia huko Bidibidi nchini Uganda wakimbizi wanufaika na mradi wa maji. Makala leo tunazungumza na vijana wa Temeke mkoani Dar es salaam nchini Tanzania walionufaika na mafunzo ya Umoja wa Mataifa, baadhi yao ni wapishi wa vyakula vya kiasili, na mashinani ni nchini SUdan Kusini kilio cha wakimbizi wa ndani wanasema hawana imani na wanasiasa na wanajeshi. Karibu basi na mwenyeji wako ni Assumpta Massoi.