Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viijana kutoka Kenya wazungumzia nafasi ya maandamano na haki za binadamu

Viijana kutoka Kenya wazungumzia nafasi ya maandamano na haki za binadamu

Pakua

Mchango wa vijana umeelezwa kuwa ni muhimu na wa lazima katika kuhakikisha haki za binadamu zinadumishwa kote dunani. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

Hayo yamesisitiuzwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake kuhusu siku ya haki za binadamu inayoadhimishwa leo Desemba 10 kote duniani. Amesema ulimwenguni kote vijana wanadamana na kikubwa ni “kupaza sauti zao katika masuala ya haki za mazingira, haki sawa kwa wanawake na wasichana , kushiriki katika kufanya maazumzi na kutoa maoni yao kwa uhuru. Wanaandamana kwa ajili ya haki yao na mustakabali wa amani, haki na fursa sawa.”

Na amesisitiza kuwa kila mtu ana haki ya kupata haki zote za kiraia, kisiasa, kiuchumi, kijamii na kitamaduni bila kujali wanaishi wapi, kabila, dini, asili yao, jinsia, mwelekeo wa kijinsia, kisiasa au maoni mengine, ulemavu au kipato, au hali yoyote ile.  Na je vijana wanaipigiwa chepuo wanasemaje? Nimezungunka katika jiji la Nairobi Kenya na kuzungumza na baadhi yao,

(MAONI YA VIJANA NAIROBI)

Katika Siku hii ya Kimataifa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amemtaka kila mtu awasaidie na kuwalinda vijana ambao wanasimama kidete kwa ajili ya haki za binadamu.

Audio Credit
UN/Jason Nyakundi
Sauti
1'25"
Photo Credit
UN/ Jason Nyakundi