Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wamiliki wa vihamba Shimbwe Juu mkoani Kilimanjaro nchini Tanzania ni mashuhuda wa manufaa ya mradi wa FAO

Wamiliki wa vihamba Shimbwe Juu mkoani Kilimanjaro nchini Tanzania ni mashuhuda wa manufaa ya mradi wa FAO

Pakua

Umoja wa Mataifa unasisitiza matumizi bora ya ardhi na kilimo endelevu kama njia mojawapo ya kuhifadhi si tu tabaka la juu la udongo wenye rutuba bali pia kuhakikisha kuwa mazao yatokanayo na kilimo hicho yanakuwa bora na yenye tija. Ni kwa kuzingatia hilo, shirika la chakula na kilimo duniani, FAO linatambua mifumu ya urithi duniani ya umiliki wa ardhi, GIAHS, ambayo inasaidia kutunza ardhi na miongoni mwao ni ule wa Kihamba au bustani  ya kifamilia mkoani Kilimanjaro nchini Tanzania. Kupitia mafunzo ya FAO, wamiliki wa vihamba sasa wanapata mazao yenye tija zaidi tofauti na awali, kulikoni? Flora Nducha basi anasimulia kwenye makala hii.

Audio Credit
UN News/Flora Nducha
Audio Duration
3'59"
Photo Credit
FAO