09 DESEMBA 2019

9 Disemba 2019

Katika Jarida la Habari hii leo Assumpta Massoi anakuletea

-Jawabu la maandamano ya kila kona duniani, ni kutokuwepo na uswwa na dawa pekee ni kuziba pengo hilo la usawa imesema Ripoti ya maendeleo ya binadamu ya UN iliyotolewa leo

-Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema asilani hatoruhusu ufisadi ukwamishe ufikiaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDGs na kuzitaka nchi kuchukua hatua kupambana na jinamizi hilo

-Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC mradi wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO wa kuelimisha jamii kuhusu ulinzi wa mtoto na ukatili wa kingono umesaidia kuongeza uelewa wa jamii kuhusu madhara ya vitendo hivyo

-Makala yetu leo inamulika  jinsi kihamba au ardhi ya kurithi kwenye familia inavyounga mkono usimamizi na matumizi bora ya ardhi

-Na mashinani leo tutapata ujumbe kutoka kwa Bw. Victorin Laboudallon, mhifadhi wa mazingira kwenye kisiwa cha Seychelles

Audio Credit:
UN News/Assumpta Massoi
Audio Duration:
11'3"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud