04 Desemba 2019

4 Disemba 2019

Mabadiliko ya tabianchi, majanga na vita vimeendelea kuwa kichocheo kikubwa cha ongezeko la mahitaji  ya kibinadamu duniani na hii leo huko Geneva, Uswisi, Umoja wa Mataifa umezindua ombi la dola bilioni 29 kunusuru wakazi wa dunia mwakani 2020. UNICEF nayo yatoa ombi lake kunusuru watoto na huko CAR wakimbizi warejea nyumbani wakitokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Makala tunabisha hodi Uganda na mashinani pia tunasalia huko huko Uganda kwa mwalimu Joy akimulika shule ya msingi iliyo jumuishi. Karibu na mwenyeji wako ni Flora Nducha.

Audio Credit:
Flora Nducha
Audio Duration:
11'8"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud