Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania inatekeleza kwa vitendo mkataba wa haki za watu wenye ulemavu- Mbunge Amina

Tanzania inatekeleza kwa vitendo mkataba wa haki za watu wenye ulemavu- Mbunge Amina

Pakua

Leo ni siku ya watu wenye ulemavu ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa ujumbe wake akisema kuwa, “tunapolinda haki za watu wenye ulemavu, tunasonga mbele kufikia ahadi kuu ya Ajenda ya 2030 - kutowaacha yeyote nyuma,”  akisema kuwa, hata hivyo bado kuna mengi ya kufanya, tumeona maendeleo muhimu katika kujenga ulimwengu jumuishi kwa wote.

Katibu Mkuu amesema takribani nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa zimeridhia Mkataba wa Haki za watu wenye Ulemavu na hivyo anawahimiza wale ambao bado hawajafanya hivyo kuuridhia bila kuchelewa.

Miongoni mwa nchi zilizoridhia mikataba hiyo ni Tanzania ambako kwa kiasi kikubwa inapiga hatua katika ujumuishaji wa watu wenye ulemavu .Akizungumza nami kwa njia ya siku kutoka kwenye maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu mjini Arusha Tanzania mbunge anayewakilisha watu wenye ulemavu Amina Molell aamesema ulemavu sio kulemaa hiyo ni dhana potovu na wanachohitaji ni ushirikishwaji na ujumuishwaji.

(MAHOJIANO NA AMINA MOLLEL)

Audio Credit
Flora Nducha/Amina Mollel
Audio Duration
3'15"
Photo Credit
UN News