Skip to main content

Wajasiriamali wa shughuli rafiki kwa mazingira Tanzania kutunzwa

Wajasiriamali wa shughuli rafiki kwa mazingira Tanzania kutunzwa

Pakua

Wakati nchi wanachama wa mkataba wa kimataifa wa mabadiliko ya tabianchi, COP25 wakikutana huko Madrid, Hispania, nchini Tanzania mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na wadau wameaandaa maonyesho ya siku mbili yatakayoleta pamoja wajasiriamali wanaotekeleza miradi mbalimbali ya kukabiliana au kuhimili mabadiliko ya tabianchi.

Akizungumza na waandishi wa  habari hii leo mjini Dar es salam, Tanzania, mwakilishi wa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP nchini humo Clara Makenya amefafanua kwa kina..

(Sauti ya Clara Makenya)

Bi. Makenya ameenda mbali zaidi kufafanua zawadi kwa mshindi..

(Sauti ya Clare Makenya)

Maonyesho hayo yameandaliwa na shirika la kazi duniani, ILO, UN Global Compact, UNEP na chama cha warejelezaji Tanzania, TaRA.

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
1'37"
Photo Credit
UNIC/Stella Vuzo