19 NOVEMBA 2019

19 Novemba 2019

Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Arnold Kayanda anakuletea

-Zaidi ya watu milioni 673 bado wanajisaidia katika maeneo ya wazi kwa kukosa huduma za vyoo umeonya Umoja wa Mataifa katika siku ya choo duniani na kuongeza kuwa choo sio tu kinaokoa maisha bali kinatengeneza maisha.

-Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limesema zaidi ya watu milioni 2.4 wanahitaji msaada wa chakula ukanda wa Sahel ya Kati

-Kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo UNCTAD imezishauri  nchi masikini kuelekeza zaidi fedha za misaada kwenye mipango ya maendeleo

-Makala yetu inatupeleka Kenya kwa mwanamke Miriam Njeri aliyejitosa katika biashara ya kushona na kuunza viatu

-Na mashinani tuko Bahrain ambako kongamano la kimataifa za ujasiriamali na uwezeshaji wa wanawake na vijana limemalizika hivi karibuni utamsikia mshiri kutoka Kenya alichojifunza na atakavyotumia elimu aliyopata.

Audio Credit:
UN News/Arnold Kayanda
Audio Duration:
10'59"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud