Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutana na Meja Veronica Owuor, afisa wa jeshi la anga kutoka Kenya sasa akihudumu Umoja wa Mataifa

Kutana na Meja Veronica Owuor, afisa wa jeshi la anga kutoka Kenya sasa akihudumu Umoja wa Mataifa

Pakua

Kutana na mwanamke shupavu, mlinzi wa amani na afisa mafunzo ya kijeshi kwenye operesheni za amani za Umoja wa Mataifa.

Meja Veronica Owuor ambaye ni afisa wa ununuzi na masuala ya kiufundi katika jeshi la anga la Kenya , lakini kwas asa ni miongoni mwa wanawake wawili tu na pekee kutoka barani Afrika wanaofanyakazi katika idara ya maafisa wa mafunzo ya kijeshi kwenye Umoja wa Mataifa.

Alipotutembelea katika ofisi zetu za UN News kwenye ghorofa ya 11 makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani alipata fursa ya kukutana na wafanyakazi wa lugha mbalimbali waliokuwa na hamasa kubwa ya kujua anachokifanya.

Na ndipo nikaambayana naye Meja veronica na kuketi katika mazungumzo ambapo amenieleza ni kwa nini aliipenda sana kazi hii ya jeshi na kutoa mafunzo

(SAUTI YA MEJA VERONICA)

Nimemuuliza Meja Veronica ni changamoto gani kama mwanamke anayefundisha idadi kubwa ya wanaume kwenye operesheni za ulinzi amani anakumbana nazo.

(SAUTI YA MEJA VERONICA)

Photo Credit
UN