Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watapisha vyoo afya zao ziko mashakani- Ripoti

Watapisha vyoo afya zao ziko mashakani- Ripoti

Pakua

Hatma ya wafanyakazi katika sekta za usafi  na hususani watoa huduma ya kutapisha vyoo kwenye nchi zinazoednea ni suala linalostahili kushughulikiwa kwa dharura kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, ukionya kuwa haki zao, afya na hadhi zao ziko hatarini. Jason na Nyakundi na maelezo zaidi.

Likiangazia hatari inayowakumba mamilioni  ya watu wanaosafisha vyoo au watapisha vyoo, mabomba na matenki ya maji taka, kabla ya kaudhimishwa siku ya choo duniani Jumanne  Novemba 19, shirika la afya duniani WHO linasema licha ya kuwa watu hao wanafanya kazi muhimu ya umma, afya zao ziko hatarini na wakati mwingi wao hutengwa.

Taarifa ya WHO iliyoambatana na ripoti mpya imesema wafanyakazi hao mara nyingi hukaribiana na uchafu wa kinyesi cha binadamu, nahufanya kazi bila ya vifaa au kinga kwa kutumia mikono yao, suala ambalo huwaweka kwenye hatari ya kuambukizwa magonjwa mengi.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa wakati tu huduma hiyo muhimu inapofeli, wakati jamii inakumbana na kinyesi cha binadamu  kwenye mitaro, mitaani na kwenye mito au wakati vyombo vya habari vinaangazia kifo cha mfanyakazi wa usafi wa kutapisha vyoo ndipo hatma zao zinawekwa wazi.

Juma ng'ombo ni mfanyakazi wa majitaka kutoka Temeke, Dar es salaam nchini Tanzania.

(Sauti ya Juma Ng'ombo)

Audio Credit
Flora Nducha/Jason Nyakundi
Audio Duration
2'34"
Photo Credit
WaterAid/Basile Ouedraogo