Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mafanikio ya azimio la Cairo kuhusu watu na maendeleo yatasalia finyu bila ushiriki wa vijana- Restless Development

Mafanikio ya azimio la Cairo kuhusu watu na maendeleo yatasalia finyu bila ushiriki wa vijana- Restless Development

Pakua

Mkutano wa maadhimisho ya 25 ya azimio la ICPD ukiendelea mjini Nairobi Kenya imeelezwa kuwa mchango wa vijana ni muhimu sana katika utekelezaji wake na kuhakikisha kwamba hakuna mwanamke na msichana anayesalia nyuma katika ejenda ya maendeleo endelevu.

Kauli hiyo inaungwa mkono pia na washiriki mbalimbali wa mkutano akiwemo Sima Bateyunga mshiriki kutoka shirika lisilo la kiserikali la Restless Development nchini Tanzania ambalo linajikita na masuala ya vijana. 

Anasema mkutano huo umekuja wakati muafaka kwa kuwa, “mkutano huu utakuwa na manufaa makubwa sana , wameongelea zaidi katika suala la ushirikishwaji wa vijana ambacho ni kitu kizuri sana. Kwa hiyo wameongelea kuna nini ambacho kimefanyika hadi sasa hivi kutoka miaka 25 iliyopita, ambayo inaonekana kuna vitu vimefanyika, lakini bado kuna masuala ya kuyafanyia kazi ambayo serikali zinaweza kuahidi kuwa hivyo ndio vitu watakavyotekeleza. Kwa hiyo inakuwa kama kengele ya kuwaamsha waweze kujua ni jinsi gani ya kuweza kufikia hilo”

Na anasema kubwa zaidi ni kwamba, “ni kwamba kila kitu kinachokuwa kinaongelewa ni ushirikishwaji wa vijana katika kutengeneza mprogramu, kutengeneza será, kutekeleza hizo será pamoja na kufanya ufuatiliaji na kufanya tathimini. Kwa sababu inamaana hii miradi ambayo inafanywa programu ziweze kuwashika vijana ni vizuri wakawa wameshirikishwa ndio itakuwa rahisi.”

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
1'19"
Photo Credit
UN Photo/Laura Jarriel