Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tutimize kile tulichokubaliana Cairo mwaka 1994- Dkt. Kanem

Tutimize kile tulichokubaliana Cairo mwaka 1994- Dkt. Kanem

Pakua

Miaka 25 ilityopita dunia iliweka ahadi ya kuhakikisha afya ya uzazi kwa wanawake na wasicha inakuwa ni haki ya msingi ili kuwawezesha kuwa huru na kufanya maamuzi ya maisha yao. Sasa umewadia wakati wa kutimiza ahadi hiyo kwa mujibu wa mkurugenzi mtendaji wa shirika la idadi ya watu duniani UNFPA, Dkt. Natalia Kanem. Priscila Lecomte na ripoti kamili.

Dkt. Kanem ameyasema hayo katika mkutano wa maadhimisho ya miaka 25 ya azimio la ahadi hiyo ya ICPD mjini Nairobi Kenya na kumbusha kwamba , miaka 25 iliyopita dunia ilikuwa mahali tofauti sana, simu ya rununu ilikuwa inaenea ndani ya mkomba, lakini leo hii dunia nzima inaenea katika simu ya rununu.

Pia amesema miaka hiyo 25 iliyopita watu walikuwa wanaendesha magari, leo hii magari yanaweza kuendesha watu. Wakati huo wanasayansi walianza kuweka data za viasili nasaba na sasa unaweza kubaini kiasili nasaba chako mwenyewe.

Dkt. Kanem amesisitiza kuwa kuna hatua kubwa zilizopigwa katika maeneo mengi lakini anahoji “Kwa nini hatushuhudii hatua hizo kubwa katika amasuala ya afya ya wanawake na haki zao, wakati miaka 25 iliyopita viongozi wa dunia walikubaliana kuwa afya ya uzazi na haki ni kipaumbele cha dunia?.

Audio Credit
Flora Nducha/Priscilla
Audio Duration
2'40"
Photo Credit
UNFPA/Georgina Goodwin