Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tutimize ahadi tuliyoweka Cairo ili kunusuru wanawake na wasichana- UN

Tutimize ahadi tuliyoweka Cairo ili kunusuru wanawake na wasichana- UN

Pakua

Hatua iliyopigwa kwa miaka 25 tangu kupitishwa azimio la kihistoria la Cairo 1994 la hatua za kumkomboa mwanamke na mtoto wa kike bado mchakato ni tete na mamilioni wanaachwa nyuma amesema naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini Nairobi Kenya.   Assumpta Massoi na maelezo zaidi.

Akizungunmza hii leo mjini Nairobi Kenya katika maadhimisho ya 25 tangu kupitishwa azimio hilo la Cairo Bi. Amina J. Mohammed amesema “mtazamo wa azimio hilo ulikuwa na bado uko bayana kuwawezesha wanawake na wasichana kupata haki zao ili waweze kudai uhuru wao, afya na ustawi wao kwa ajili ya faida za muda mrefu za familia zao, jamii zao na mataifa yao.”

Amesema licha ya hatua kubwa zilizopigwa kutokana na kujitolea na kazi iliyofanywa katika shughuli na kampeni mbalimbali  cha kusikitisha wakati tukitathimini hayo cha kusikitisha  ni kwamba mchakato huu ni tete na mamilioni ya wanawake na wasicha unawaacha nyuma. Hivyo amesema“Tunahitaji kuongeza hatua haraka kutekeleza mpango wa hatua wa azimio hilo ili kutimiza malengo ya maendeleo endelevu. Hili ni muhimu wakati tukiingia katika muongo wa hatua za kufanikisha SDGs.”

Amesisitiza kwamba dunia bado ni ngumu na mara nyingi ni mahali pa hatari kwa mamilioni ya wanawake na wasichana. Na ili kufanya isiwe ngumu zaidi ,viongozi katika maeneo yote wanahitaji kuboresha utekelezaji wa ahadi za Cairo, za kupata mustakabali mzuri kwa vijana wetu haswa wasichana wetu. Na kwamba“kama wachagizaji wa malengo ya maendeleo endelevu , matokeo ya mpango huu wa kuchukua hatua ni lazima uendelezwe. Mkakati wetu wa pamoja kwa ajili ya watu , kwa ajili ya sayari yetu , ustawi , amani na ushirika vinategemea hilo”

Ameongeza kuwa mustakabali endelevu utawezekana tu endapo ahadi iliyowekwa kwa mamilioni ya wanawake na wasichana miaka 25 iliyopita itatimizwa.

Hivyo amesema, "nategemea kila mmoja wenu na kwa pamoja kutimiza ahadi, kulinda mustakabali wa wasichana wetu na kuwawezesha wanawake."

Audio Credit
Flora Nducha/Assumpta Massoi
Audio Duration
2'15"
Photo Credit
Diana Nambatya/Photoshare