11 Novemba 2019

11 Novemba 2019

Hii leo jaridani Flora Nducha anaanzia nchini Kenya ambako msaada wa chakula umepelekwa kaunti za Mandera, Wajir, Garissa na Tana River ambako mafuriko yameleta adha. Kisha Sudan  Kusini wanafunzi wa shule moja ya msingi angalau wapata nuru mpya shuleni kufuatia ujenzi wa madarasa kupitia mradi wa matokeo ya haraka unaotekelezwa na UNMISS. FAO nayo na mfuko wa mazingira waanzisha mradi wa kusaidia mataifa kuwa na takwimu sahihi za misitu. Makala tunakwenda nchini Uganda ambako utasikia kuhusu manufaa ya nyuki kwa uzalishaji wa chakula na mashinani tunabisha hodi Yemen. Karibu!

Audio Credit:
Flora Nducha
Audio Duration:
11'19"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud