08 Novemba 2019

8 Novemba 2019

Leo Ijumaa ni mada kwa kina tukimulika harakati za Kenya kupata uwakilishi usio wa kudumu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na mgeni wetu ni Waziri wa Mambo ya Nje Monica Juma. Hata hivyo tunamulika pia habari nyingine tunamulika huko pembe ya Afrika na operesheni za kusaidia manusura wa  mafuriko Somalia na Sudan Kusini kisha tunakwenda Haiti nako hali si shwari na pia tunamulika uchumi ukanda wa Afrika Mashariki. Mhadhiri Vincent Leyaro kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam nchini Tanzania anabainisha chanzo cha pengo la ajira kwenye  ukanda huo  unaokua kwa kasi kiuchumi. Neno la wiki, BAKIZA leo wanafahamisha maana ya neno Radhi. Karibu na mwenyeji wako ni Assumpta Massoi.

Audio Credit:
Assumpta Massoi
Audio Duration:
9'55"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud