07 Novemba 2019

7 Novemba 2019

Hukumu ya John Bosco Ntaganda iliyotolewa leo huko The Hague ndio habari yetu muhimu ikifuatiwa na huko Sudan  Kusini, Umoja wa Mataifa na wadau wafika kambi ya kikundi cha SPLA upande wa upinzani kuona iwapo wanatumikisha watoto na wanawake vitani au la, kisha tunabisha hodi Uganda, ambako serikali ya Japan imeunga mkono hatua za Umoja wa Mataifa kwa kujenga maabara ya kwenye shule ya sekondari katika makazi ya wakimbizi ya Kyangwali mjini Hoima. Makala ni UNDP na Tanzania zafanikisha utoaji wa hati za kumiliki ardhi kimila kijiji cha Magunga mkoani Tanga na mashinani tunabisha hodi Yemen. Karibu na mwenyeji wako ni Assumpta Massoi.

Audio Credit:
Assumpta Massoi
Audio Duration:
13'1"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud