Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ingawa mradi ulimalizika, wanawake India walisimama kidete na sasa wamejikwamua

Ingawa mradi ulimalizika, wanawake India walisimama kidete na sasa wamejikwamua

Pakua

Rais wa mfuko wa maendeleo ya kilimo wa Umoja wa Mataifa Gilbert Houngbo akiwa ziarani India ametembelea miradi ya IFAD inayowawezesha wanawake wa vijijini nchini India.

Akiwa amevalia kilemba cha kitamaduni katika jimbo la Maharashtra, bwana Houngbo ametembelea miradi inayofadhiliwa na IFAD ya kundi la Tejaswini ya wanawake wa kuwezesha wanawake wa vijijini kwa ajili ya kushuhudia mabadiliko katika maisha na vyanzo vya vipato kwa takriban wanawake milioni moja wa vijijini, “unajua wakati tunazungumzia wajibu wa IFAD kuwa ni kubadili maisha vijijini na kubadili uchumi vijijini, haya ndio tunayozungumzia.”

Licha ya kwamba mradi huo ulitekelezwa na kukamilia mwaka 2018 lakini umeendelea kusaidia wanawake katika vikundi vya kujitegmea kwa kuwawezesha kupata huduma za benki, mafunzo ya kilimo, elimu na mafunzo ya kuendesha biashara na maendeleo ambapo rais Hungbo hakuficha hisia zake, “imekuwa karibu miaka miwili au mitatu sasa tangu mradi ulifungwa na kushuhudia maendeleo ya mradi na umiliki wa mradi sio hasa wa IFAD ni wa wanawake, ni juhudi za wanawake mashinani.”

Tangu mradi karibu wanawake milioni moja walioshiriki mradi huo wa IFAD, asilimia 64 wameongeza maradufu vipato vyai kutokana na mradi lakini si tu fedha zaidi lakini kuna mengine kama anavyosema Manjula Gurunth Patil mfugaji wa ng’ombe wanaozalisha maziwa, "Awali, wanawake walioolewa walikuwa wanasalia nyumbani, ni baada ya kujiunga na kundi la kuwezesha wanawake ambapo niligundua kuwa kuna Maisha nje ya kuta nne za nyumba na kwamba hakukuwa na haja ya kuwa gizani.”

Rais Houngbo alitembelea pia Kijiji cha Vadayali ambako wanawake walionyesha shughuli zao na kuzungumzia mafanikio na changamoto zao.

IFAD imesema iko njia sahihi na inahitaji kuendelea kutoa kipaumbelea kwa miradi inayozingatia jinsia na kwamba changamoto ni kuongeza miradi sio tu katika ukanda lakini kote ndani na nje mwa India.

Audio Credit
Arnold Kayanda/Brenda Mbaitsa
Audio Duration
2'21"
Photo Credit
IFAD