30 Oktoba 2019

30 Oktoba 2019

Hii leo jaridani, Arnold Kayanda anaanza na ripoti za uzinduzi wa kamati ya kikatiba kwa taifa la Syria huko Geneva, Uswisi! Imeelezwa kuwa ni tukio la historia. Atakwenda pia India kuona jinsi uaminifu wa wanawake wa vijijini  umesaidia mradi uliokuwa  umemalizika muda wake uendelee kuwa na manufaa kwa wanawake hao wa vijijini na familia zao. Nchini Ethiopia nako wenyeji na wakimbizi wapatiwa stadi za pamoja za kazi k ufuatia msaada kutoka Ujerumani na sasa wanaona nuru katika maisha yao. Makala ni mkoani Morogoro, kijana wa kike aanzisha shirika la kiraia la kukwamua wanawake na mashinani leo tunaye Kanali Dokta Agatha-Mary Katua kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania, JWTZ akipaza sauti kwa wanawake na wasichana. Kulikoni? Karibu!

Audio Credit:
Arnold Kayanda
Audio Duration:
9'56"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud