28 Oktoba 2019

28 Oktoba 2019

Hii leo jaridani, Arnold Kayanda anaanza na mkutano wa masafa ya redio unaofanyika huko Misri, kisha anamulika jinsi gani makazi ya kuelimisha waume na waume watarajiwa yamesaidia kuondoa mikwaruzano kwenye ndoa huko Burkina Faso. Anamulika pia watoto wawili wa kike maswahiba wakubwa huko Uganda, ni wakimbizi kutoka DRC lakini sasa wanasaidiana kimasomo. Makala tunabisha hodi Morocco mradi wa IFAD na mashinani ni ushauri wa Dkt. Mukhisa Kituyi, Katibu Mkuu wa UNCTAD kuhusu nini kifanyike nchi za Afrika zinufaike zaidi na teknolojia ya kidijitali, karibu!

Audio Credit:
Arnold Kayanda
Audio Duration:
9'54"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud