Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana Kenya wasimama kidete kunufaika na mradi wa uchimbaji mafuta Turkana

Vijana Kenya wasimama kidete kunufaika na mradi wa uchimbaji mafuta Turkana

Pakua

Nchini Kenya, kugundulika kwa mafuta kaskazini mwa nchi hioyo kumefungua fursa za kipato si tu kwa kampuni bali kwa wakazi wa kaunti ya Turkana iliyoko eneo hilo. Wanawake, wanaume na vijana wameitikia wito wa Umoja wa Mataifa wa kuchangamkia fursa ili kutekeleza miradi ya uhifadhi wa mazingira hususan kwenye maeneo ya machimbo ya mafuta. Miongoni mwa walioitikia wito wa ni vijana wa Turkana ambao kupitia kikundi chao wananufaika bila hata kuajiriwa na kampuni ichimbayo mafuta ya Tullow. Mwandishi wetu John Kibego amezungumza na kijana Mark Mangiro, Mratibu wa kikundi hicho cha Kapese Young Stars kuhusu jitihada zao za kunufaika na ugunduzi wa mafuta bila kuajiriwa moja kwa moja  na kampuni hiyo.

Soundcloud
Audio Credit
Brenda Mbaitsa/John Kibego
Sauti
3'45"
Photo Credit
Photo: IRIN/A. Morland