15 Oktoba 2019

15 Oktoba 2019

Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Assumpta Massoi anakuletea

-Ripoti iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF inasema lishe na mifumo duni ya vyakula inaathiri afya na ukuaji wa mamilioni ya watoto duniani

-Watu milioni 800 kote duniani wanakabiliwa na njaa na kutomudu mahitaji ya lazima ya chakula limesema shirika la WFP katika kuelekea siku ya chakula duniani

-Msanii mashuhuria na balozi mwema wa UNICEF Angelique Kidjo amegawa viatu kwa wasicha mashuleni nchini Benin na kusema ni sehemu kubwa ya kuwachagiza watoto kwenda shuleni

-Makala leo inatupeleka Karagwe mkoani Kagera Tanzania kummulika mwanamke wa kijijini siku yao ikiadhimishwa

-Na mashinani utamsikiamkulima wa mpunga kutoka Gambia ambaye ni mnufaika wa mradi wa shirika la kimataifa la ufadhili wa maendeleo ya kilimo IFAD.

Audio Credit:
UN News/Assumpta Massoi
Audio Duration:
10'46"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud