Licha ya changamoto, mashirika ya posta ya zamani bado yanajitahidi kuendelea na huduma

9 Oktoba 2019

Ulimwengu unapoadhimisha Siku ya Posta Duniani hii leo, mashirika ya posta kwenye nchi nyingi yameathirika tangu ya kuibuka kwa teknolojia za mawasiliano hasa ya simu za mkononi. Lakini licha ya hilo mengi yamejikakamua na kubuni mbinu mpya hususan za  kuitumia teknolojia ile ile mpya ya mawasiliano kuendelea kutoa huduma. Sherehe za maadhimisho hayo zimefanyika nchi nyingi na mwandishi wetu nchini Kenya  Jason Nyakundi alihudhuria maadhimisho hayo mjini Nairobi ambapo amezungumza na Meneja Mkuu wa mawasiliano kwa njia ya barua katika shirika la posta la Kenya Milka Kagwe kuhusu jinsi posta imenufaika na teknolojia mpya.

Audio Credit:
Jason Nyakundi
Audio Duration:
5'30"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud