09 Oktoba 2019

9 Oktoba 2019

Hii leo habari yetu kubwa ni kuhusu utafiti uliofichua jinsi wanawake wanavyokumbwa na mateso wanapokuwa wanajifungua, makaripio, kukemewa na kadha wa kadha. Kisha ni harakati za kukabili mlipuko wa surua huko DR Congo, ugonjwa ambao sasa ni tishio kuliko hata Ebola. Nchini Kenya, muziki waunganisha vijana kutoka mataifa mawili tofauti na katika makala leo siku  ya posta duniani ni jibu mahsusi kwa wale wadhaniao kuwa teknolojia imechimbia kaburi huduma za kutuma barua na vifurushi na mashinani ni ujumbe wa UNCTAD kwa viongozi wa Afrika. Karibu na mwenyeji wako ni Arnold Kayanda.

Audio Credit:
Arnold Kayanda
Audio Duration:
10'54"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud