08 Oktoba 2019

8 Oktoba 2019

Je wafahamu kuwa watu bilioni 2.2 wanapata upofu au uoni hafifu ilhali wanaweza kuepuka shida hiyo? Ni miongoni tu mwa habari zetu za leo kwenye Jarida la Habari za UN likiletwa kwako na Flora Nducha. Taarifa nyingine ni mtoto mkimbizi kutoka Sudan Kusini ahaha kuhakikisha anafanikisha ndoto zake ingawa yu ukimbizi DR Congo. Kisha tunamulika kijana aliyeazimia kutokomeza ajira miongoni mwa watoto kwa kuwa naye ni manusura. Makala inabisha hodi Zimbabwe? tamu na chungu kutoka kwa wanawake na wasichana waathirika na wanufaika wa mipango ya afya ya uzazi ikiwa ni kuelekea ICPD 25. Mashinani tuko Somalia, karibu!

 

Audio Credit:
Flora Nducha
Audio Duration:
13'2"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud