Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

07 Oktoba 2019

07 Oktoba 2019

Pakua

Hii leo jaridani na Flora Nducha anaanzia Geneva Uswisi ambako suala la wakimbizi lajadiliwa na UNHCR yahoji mpaka lini wakimbizi watakuwa wanapigwa'danadana?' kisha anabisha hodi huko Ethiopia mwalimu mkimbizi aamua kushika chaki ili kuendelea na kazi hiyo aipendayo na baada ya hapo anakwenda Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, wakimbizi wa ndani waliofurushwa makwao wasaka hifadhi karibu na kambi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa na makala leo tunabisha hodi huko nchini Kenya, wanawake na ubunifu katika makazi duni ikiwa leo ni siku ya makazi duniani bila kusahau mashinani. Karibu!

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
12'7"