Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania, Burundi na Kenya na ujumbe wao kwa Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la UN, UNGA74

Tanzania, Burundi na Kenya na ujumbe wao kwa Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la UN, UNGA74

Pakua

Sasa ni mada kwa kina tukimulika kile ambacho Kenya, Burundi na Tanzia zimewasilisha mbele ya viongozi w anchi 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa wakati wiki hii ya mjadala mkuu kwa lengo la kufanikisha ajenda ya maendeleo endelevu SDGs sambamba na amani, usalama na haki za binadamu. Na moja basi ya masuala ambayo yamejadiliwa katika mikutano ya ngazi ya juu wiki hii ni huduma ya afya kwa wote ambapo Kenya ni moja ya nchi ambazo zimezindua mkakati huo katika kaunti nne kati ya kaunti 47 nchini mwake ambapo rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta amezungumzia mikakati ambayo wameweka kuhakikisha afya kwa wote ambapo rais Kenyatta anafafanua mkakati huo na lengo la kuhakikisha kwamba kila mwananchi anapata hudumua ya afya bila malipo. Kutoka Kenya tunamulika Burundi ambapo Waziri wa mambo ya nje ya Burundi Ezechiel Nibigira anaeleza kwamba hivi sasa warundi wameshaelewa kuwa nchi yao inapaswa kujitegemea na hivyo wote kwa pamoja wameanza kupambana na umaskini na tayari wanaanza kutoka kwenye giza kuelekea kwenye nuru. Kwa upande wa Tanzania  Profesa Palamagamba John Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika MAshariki, ambaye amezungumza na Assumpta Massoi akifafanua ujumbe wao kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Audio Credit
Arnold Kayanda/ Uhuur Kenyatta/ Ezechiel Nibigira/ Palamagamba John Kabudi
Audio Duration
6'27"
Photo Credit
UN Photo/Amanda Voisard